-->

Watengeneza kisiwa cha udongo ili wanywe pombe pasipo kukamatwa na Polisi

Kutokana na marufuku dhidi ya unywaji pombe hadharani wakati wa sherehe za mwaka mpya nchini New Zealand kikundi kimoja cha watu kutoka eneo la kisiwa cha Coromandel nchini humo kimeshangaza watu baada ya kutengeneza kisiwa kidogo cha udongo kisiwani hapo ili wanywe pombe bila kukamatwa na polisi kwa kukiuka marufuku hiyo.

Kwa mujibu wakazi hao, walitengeneza kisiwa hicho wakati maji yamekupwa ili wanywe pombe kwa uhuru kutokana na kwamba hilo ni eneo la bahari la kimataifa ambalo halimilikiwi na taifa lolote hivyo wasingekamatwa na vyombo vya dola.

Kamanda wa Polisi wa eneo hilo Inspekta John Kelly alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema huo ni ubunifu wa hali ya juu sana na laiti kama angelelijua suala hilo mapema angeungana nao.

chanzo : millardayo

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364