-->

Abby Skills Awashukuru Alikiba na Mr. Blue

Msanii wa Bongo Fleva Abby Skills amesema anawashukuru sana wasanii Ali Kiba pamoja na Mr. Blue kwa kumrejesha kwenye game la muziki baada ya kupotea kwa miaka minne mfulilizo.

mr-blue23

Abby ameyasema hayo alipokuwa katika kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV ambapo pia alitambulisha ngoma yake mpya na video yake inayokwenda kwa jina la ‘Averina’ ngoma ambayo amewashirikisha Ali Kiba pamoja na Mr. Blue.

“Ninawashukuru sana Ali Kiba pamoja na Mr. Blue kwa kunirudisha kwenye game , ni watu ambao tumekuwa pamoja na wameisapoti sana kazi yangu hii” Amesema Abby

Kwa upande wake Mr. Blue amesema Abby Skills ni mtu muhimu sana katika maisha yao ya muziki hivyo wapo naye na watazidi kushirikiana naye katika mambo mbalimbali.

Pamoja na hayo Abby amesema pamoja na kuwa nje ya game kwa muda wote lakini hajawahi kukata tamaa na kujiingiza kwenye vitendo vya madawa ya kulevya kama ilivyo kwa wasanii wengine na kusisitiza kwamba ataendelea kupambana ili kuhakikisha anarejea kwenye game kama zamani na kuwataka mashabiki kumuunga mkono kwa kazi anazofanya.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364