Ujumbe wa Francis Cheka Baada ya Taarifa za Kifo cha Thomas Mashali
Wiki hii imeanza kwa huzuni kwa mashabiki wa mchezo wa ngumi nchini baada ya kifo cha bondia Thomas Mashali hasa baada ya kusikia taarifa za chanzo cha kifo hicho. Mmoja wa watu walioumizwa na taarifa hizo ni Francis Cheka.
Kupitia mtandao wa Instagram, Cheka ameandika:
Ilikuwa ni heshima kuingia ulingo mmoja na wewe ndugu yangu Thomas Mashari,
tulipanga tukutane tena 26/11, kweli hakuna aijuae kesho…
ila Mungu tu…
Ulale mahali pema peponi ndugu yangu, Mungu akutangulie…
We unatangulia si tunafuata,
Kila nafsi itaonja mauti…
Jina la Bwana lihimidiwe.
Wawili hao walikuwa ni wapinzani kwenye mchezo huo na wamefanikiwa kucheza mapambano kadhaa lakini Cheka amefanikiwa kuibuka mshindi kwenye mapambano mengi zaidi.