-->

Abdu Kiba: Sioni Sababu ya Kiba Square Kuja Sasa

Msanii Abdukiba mdogo wa Alikiba amefunguka na kusema kuwa kwa sasa haoni sababu ya kazi zao kama kundi na kaka yake kuanza kutoka kutokana na Alikiba kuwa na kazi nyingi za kushirikiana hivyo atasikika kwa muda mrefu katika kazi mbalimbali.

ABDULI

Abdu Kiba alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz ya EATV na kusema kutokana na Alikiba kuwa na kazi nyingi sana hivyo ameona yeye saizi bora atoke na Mr. Blue ili kuleta utofauti maana Alikiba atakuwa amesikika kwenye kazi nyingi sana na kushirikishwa.

” Siyo kweli kusema Alikiba hanipi support anatoa support kubwa sana kwangu sema watu hawajui tu, Kiba Square ipo na kazi zipo ila kwa sasa hatuwezi kusema tuachie kazi maana kuna kazi nyingi za Alikiba za kushirikishwa zitatoka hivyo atakuwa anasikika kwenye kazi nyingi, ndiyo maana nikaona mimi saizi nitoke na Mr Blue, harafu tutakuja kutoka na Kiba Square” alisema Abdu Kiba

Mbali na hilo Abdu Kiba alifafanua namna ambavyo watu walimwelewa vibaya baada ya kusema yupo tayari kufanya kazi na WCB Wasafi, akisema kuwa yeye anaweza kufanya kazi na WCB Wasafi kibiashara kama kufanya show, collabo lakini si kuhamia au kusimamiwa na label hiyo

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364