-->

Acha Wajichore , Aunt Ezekile, Kajala, Chuchu Hans, Nuh Mziwanda, Harmonise

KATIKA dunia ya sasa ya mwendo kasi suala la watu kujichora tattoo sio jambo geni. Wapo wanaojichora kwa ajili ya kuwaenzi wenza wao kwa maana wapenzi, wao, watoto na hata familia zao. Huchora picha ama majina na hata herufi za wahusika mradi kuonyesha namna wanavyowazimia na kuwajali. Kwa mfano katika soka, nyota wa kimataifa wa Sweden, aliyetangaza kustaafu kuichezea nchi yake, Zlatan Ibrahimovic ana michoro 14 tofauti mwilini mwake.

SHILOLE99

Kwa kuwa dunia ya leo ni kama kijiji, baadhi ya mastaa wa Tanzania wameingia kwenye mkumbo wa kujichora tattoo, nyingine za kuonyesha mahaba yao kwa wenzao wao na nyingine kama shukrani kwa kile walichofanyiwa na watu ama rafiki zao za karibu.

 

Mwanaspoti linakuletea orodha ya mastaa ambao waliojichora tattoo za wasanii wenzao kwa kuashiria mahaba mazito waliyonayo kwao pamoja na shukrani kwa mazuri waliyofanyiwa na waliowaandika au kuyachora majina yao.

AUNTY EZEKIEL

Diva kutoka katika kiwanda cha filamu nchini, Aunty Ezekiel a.k.a Mama Cookie aliyewahi kuhusishwa kutoka na tajiri Jack Pemba na Hartmann Mbilinyi kabla ya kuolewa na Sunady Demonte, kafa kaoza kwa mwenza wake wa sasa, Moze Iyobo.

Kimwana huyo amejichora tattoo mgongoni mwake yenye jina la mzazi mwenzie huyo waliyebahatika kupata naye binti aitwaye Cookie, chini ya jina la mtoto huyo.

CHUCHU HANS

KATIKA hali inayoonesha mahaba yamemkolea dhidi ya mwenza wake, Vincent Kigosi ‘Ray’, mwigizaji Chuchu Hans ameamua kuugeuzi mwili wake kama pambio kwa kuandika jina la waubani wake.

Chuchu amejichora tattoo inayosomeka kwa jina la Ray, huku Ray naye akijiandika jina la Chuchu Hans. Wacha mahaba yawaue bhana!

NUH MZIWANDA

Kipindi cha mahaba niue baina yake na Shilole, Nuh Mziwanda ilikuwa ngumu kumwambia chochote kwa mwimbaji na mwigizaji huyo. Alikufa na kuoza kwa Shilole, kiasi cha kufikia hatua ya kujichora mkononi tattoo ya sura ya Shilole na maneno ya Shishi baby, huku Shilole naye akiliandika jina la Nuh juu ya kifua chake, kuonyesha mahaba yake kwa king’asti wake.

Hata hivyo, wawili hao kwa sasa wamemwagana, kila mtu sasa akila raha zake katika kiota kipya cha mahaba na tayari Shilole ameshafuta tattoo ya Nuh iliykuwa kifuani na Nuh ameshapata mpenzi mpya ambaye atamfanya afute tattoo yake.

HARMONIZE

Chipukizi huyu wa muziki wa kizazi kipya kutoka Lebo ya WCB inayomilikiwa na staa wa kimataifa, Diamond Platinumz, amechora tattoo ya picha ya Diamond Platnumz kwenye mkono wake na kuandika jina la Simba.

Harmonize alisema katika maisha yake hakuwahi kuwaza kama itatokea siku akajichora tattoo, lakini kutokana na mchango wa Diamond hana jinsi.

Mwimbaji huyo alisema kwa jinsi alivyothaminiwa na Diamond akiwa ametoka katika manyanyaso na kudharaulika, anaona hana jinsi ila kujichora mchoro huyo.

KAJALA

Mwigizaji mwingine wa filamu nchini, Kajala Masanja naye yumo katika orodha hii baada ya kuonyesha shukrani zake kwa shoga yake wa zamani, Wema Sepetu. Kajala aliamua kuandika jina la Wema mgongoni mwake, baada ya Madame kumuokoa asiende kuozea jela kwa kumlipa Sh. 13 milioni baada ya kukutwa na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na mwenza wake ya utakatishaji wa fedha mwaka 2013.

Kajala aliwahi kusema aliamua kujichora jina la Wema kama ishara ya kuonyesha shukrani kwa msanii mwenzake huyo, kabla ya wawili hao kutibuana na kuwa kama paka na chui.

DARK MASTER

Rapa memba wa Kundi la Chamber Squad, amejichora tattoo yenye majina ya marehemu Ngwea na Geez Mabovu.

Dark Master alikuwa mtu wa karibu na rapa hao na amedai kuwa misiba hiyo miwili ni pigo kubwa kwake, hivyo kujichora tattoo hizo ni ishara ya upendo kwa wakali hao waliotangulia mbele ya haki.

Rapa huyo ambaye alikuwa mnywaji pombe na mvutaji sigara sana kwa sasa ameamua kuokoka akiachana na vitu hivyo.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364