-->

Mkali wa ‘Digital Pastor’ Atoboa Chanzo cha Soko la Filamu Kushuka

Msanii na mtunzi wa filamu bongo anayetamba na filamu yake ya Digital Pastor Salehe Lufedha amedai kuwa chanzo cha soko la Filamu kushuka ni wasanii wa kike ambao wana majina makubwa.

Digital Pastor

Salehe Lufedha

Akizungumza Katika kipindi cha MID_MORNING TRIP (Kona ya filamu) kinachorushwa na SAFARI RADIO Lufedha amesema kwmba kwa sasa tasnia ya filamu bongo inayumba kutokana na wasanii nyota wa kike kushidwa kuthamini kazi hiyo.

“Wasanii wa kike wakishajiona mastar wanaanza kuwadharau wasanii wachanga na kusahau wao walipotoka lakini pia hishindwa kujali muda wa kufika location kwa kudhani kuwa wao ndo wamebeba tasnia”.Lufedha ameongeza kuwa kamwe hatokuja kuwatumia wasnii wenye majina katika filamu zake kutokana na wasanii hao kushindwa kujali kazi hiyo ambayo inawaweka mjini.

Hata hivyo kwa sasa salehe lufedha chini ya Kampuni yake ya Lufedha Film Co yupo chimbo kwa ajili ya maandilizi ya filamu ya The Tailer,Standard Seven pamoja na Udugu wa Nazi ambazo zitatoka baada ya mwezi mtukufu

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364