-->

Afande Aibuka Baada ya Kutajwa kwenye ‘Zilipendwa’

Msanii mkongwe wa muziki wa hop hop, Afande Sele baada ya kujwa kwenye wimbo Zilipendwa wa WCB, amedai amependezwa na kitendo hicho kwa mpongeza Diamond Platnumz.

Wimbo ‘Zilipendwa’ uliowahusisha wasanii wote wa WCB, umeibua maswali mengi kwa baadhi ya mashabiki kutokana na maudhui ya wimbo huo kwa kuwataja baadhi ya mastaa wa zamani akiwemo Afande Sele.

Afande Sele amesema hajachukizwa na kitendo cha kutajwa kwenye ‘Zilipendwa’ na kuonesha kufurahia jambo hilo mbali na wengine huku akiwaambia walioupokea vibaya msiba hauwahusu.

“Sana mdogo wangu nyakati zinabadilika huu muda wa akina Damian sio nyakati za Burning Spear au Bob Marley , ndio maana nikawa Muhenga, wamuache Dogo afanye kazi zake #safiplatnumdiamond.,” aliandika Afande Instagram.

Wasanii wengine waliotajwa kwenye wimbo huo ni H Baba, Mr Nice pamoja na wengine wengi.

Wimbo huo umeachiwa muda mchache baada ya Alikiba kutoka RockStar4000 kuachia wimbo wake mpya, Seduce Me.
Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364