Afande sele Adai Kuwa na Wanawake Kama Sita Hivi, Anawachunguza
Msanii wa muziki na mwanasiasa kutoka mji kasoro bahari, Afande Sele amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye hatarajii kuoa kwani bado yupo yupo sana ingawa anakiri wazi kuwa yupo na mahusiano na wanawake kama sita hivi ambao wanamsaidia kumtunzia watoto wake huku akiangalia kati yawatu hao alionao yupi anastahili kuwa malkia.
Afande Sele alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya Eat Africa Radio na kusema kwa sasa yeye kusema atafunga ndoa itakuwa ni uongo mkubwa kwani watu alionao anaona bado wanapimana maana wao wanampima yeye na yeye anawapima wao na kuona yupi anastahili kuingia ndani kama mke.
“Niwe mkweli tu hilo wazo la kuvuta jiko sina, namshukuru Mungu nimepata watoto wawili naweza kwenda nao vizuri na kuwalea, kusema nifunge ndoa leo au kesho utakuwa uongo sababu ndoa si kusema mwanamke kuchukua nyanya tu gengeni,lazima nipate mwanamke amabaye atakuwa na vigezo vya kuwa na mimi atajua nini maisha ambayo mimi nayahitaji, atanielewa tabia zangu za nje na ndani hivyo sidhani kama ni rahisi kupata mke kwa kipindi hiki ila najivunia kuwa na marafiki ambao wanasaidia kulea watoto wangu, wanawapenda watoto zangu hicho nashukuru” alisema Afande Sele.
“Nipo kwenye kupima nawapima na wao wananipima mimi, mimi na marafiki wa hivyo wakati ukifika nikiona yupo anafaa kuwa na mimi nitakuwa naye lakini niwe mkweli, siko mwenyewe au kusema natumia sabuni hapana mimi na warembo kama kawaida, wananisaidia kukaa na watoto wangu, wanaheshima. Maana mimi ni kama mfalme hata mfalme Suleman alikuwa wa wake zaidi ya mia tatu kwenye nyumba yake, hata mimi wapo kadhaa ila hawazidi sita” aliongeza Afande Sele
eatv.tv
NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA