-->

Afande Sele Amfungukia Mama Kanumba

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Afande Sele, amesema anashangzwa na kitendo cha Mama Kanumba kushukuru kufungwa kwa Lulu wakati mtoto wake ndiye alikuwa na makosa kwa kuwa na mahusiano na binti mdogo.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Afande Sele amesema mama Kanumba ni mama ambaye hana vigezo vya kuwa mzazi kwani hana uchungu na mtoto wa mwenzake kwenda jela akiwa mdogo, huku ambaye alistahili kuhukumiwa ni mtoto wake Kanumba.

“Mama Kanumba nimeshangaa kusikia anashukuru kwamba Lulu kafungwa, mama ambaye hana uchungu hana sifa ya kuwa mzazi, anashukuru kwamba mtoto mdogo anafungwa kwa ajili ya ubazazi wa mtoto wake, ujinga wa mwanae, upuuzi wa mwanae, mkubwa anambaka mtoto mdogo kama yule”, amesema Afande Sele.

Afande Sele ameendelea kwa kusema kwamba yeye kama mzazi mwenye mtoto wa kike anatamani hata maiti ya Kanumba ingefukuliwa ichomwe mto ili kuwa fundisho kwa wanaume wengine wenye matendo kama yake.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364