Dk Cheni Awafungukia Wanaosema Hukumu ya Lulu Haitoshi
MSANII mkongwe katika tasnia ya maigizo Bongo na mshereheshaji (MC), Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye ni mlezi wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa maoni yake kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuibuka maneno mengi kwenye mitandao hiyo ambapo watu wengine wanasema Lulu amepewa adhabu ndogo na wengine wakipendekeza angefungwa kwa miaka mitano na kuendelea.
Dk Cheni amewalaumu wasiomtakia mema Lulu akisema mambo yote mabaya yanaweza kumtokea yoyote, kwa hiyo kufurahia jambo baya limpatalo mtu si jambo jema. Pia ametoa asante kwa wote wanaomwombea mema Lulu na waendeleee kufanya hivyo.
Ujumbe aliotuma msanii huyo ni huu hapa chini:
Linapokukuta jambo wapo wataokuonea huruma na wapo watakaokuwa na furaha ila niwakumbushe jambo hakuna ajuwaye kesho yake kubwa kila mapito mwambie Mungu Asante.
Watanzania walio wengi wanakuombea yaliyo mema Tunakuahidi tupo nawe kukushika mkono kwa kila hatua Maombi yao Mungu atayasikia hata kama hukumu imepita Tupo na wewe na Mungu yupo na wewe
Chanzo:GPL