-->

Afande Sele Atoa Neno kwa Wavuta Sigara na Wanywaji wa Pombe

Msanii Afande Sele amefunguka na kusema kama Taifa tunakila sababu ya kuendelea kuwaombea watu wanaovuta sigara na walevi wa pombe kwa kuwa kila mwaka ndiyo watu ambao wanaibuka vinara kwenye kuchangia kulijenga taifa kwa mapato.

Afande Sele amesema hayo baada ya jana Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kuwasilisha bungeni mapendekezo ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2017/18 ambapo Afande Sele anakiri kuwa ni kweli bajeti hiyo ni nzuri na kusema kama Taifa halijawahi kuwa na bajeti mbaya sana bali huwa na tatizo kubwa katika utekelezaji wa mipango hiyo.

“Kweli bajeti ya mwaka huu ni nzuri sana kabisa. Ingawa kama Taifa hatujawahi kuwa na bajeti mbaya sana. Lakini tumewahi kuwa na utekelezaji mbaya sana wa malengo ya bajeti miaka yote. Mipango siyo matumizi haya basi tuendelee kuwaheshimu na kuwaombea walevi na wavutaji wasigome, wasiugue na ikibidi wasife mapema ili waendelee kuwa vinara wa kulichangia na kulijenga Taifa kupitia ongezeko la kodi kwa bidhaa zao kila mwaka” alisema Afande Sele

Afande Sele alisema haya baada ya serikali kuendelea kupandisha kiwango cha ushuru kwenye vinywaji baridi, bia pamoja na sigara.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364