-->

Afande Sele:Natamani Kuoa Tena

Mwanamuziki mkongwe kwenye muziki wa bongo fleva Afande Sele amefunguka na kusema kwa sasa anajisikia kuoa tena baada ya muda mrefu kupita akiishi mwenyewe na kutofurahia maisha anayoishi kutokana na kukosa mke.

afande selle

Afande Sele siku kadhaa zilizopita alisema kuwa yupo na marafiki kadhaa wa kike ambao wanamsaidia kulea watoto wake, na kumfanya aishi akiwa na amani kwani wanamsaidia kutunza watoto, na kudai ya kwamba yeye anaona wanachunguzana na hao mabinti ili akiona yupo mmoja wapo ambaye ana sifa ya kuwa mke bora aweze kuwa naye kama malkia kwa kuwa yeye ni mfalme.

Lakini leo kupitia ukurasa wake wa Facebook aliweka picha akiwa anakula chakula kwenye sufuria na kutoa sababu ambazo zinamfanya atamani kuoa tena, moja wapo ni uvivu wa kuosha vyombo ndiyo maana anaamua kula kwenye sufuria.

“Najisikia “kuoa” tena…Mara chache huamua kula kwenye sufuria kwa sababu naishi mwenyewe hivyo napika mwenyewe, naosha vyombo mwenyewe nk, hivyo kwasababu ya uvivu wangu katika kuosha vyombo wakati flani huamua kula kwenye sufuria ili kuepuka kuchafua vyombo, zaidi pasi na ulazima’anko magu style'” aliandika Afande Sele

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364