-->

Nay wa Mitego Ahofia Kufungiwa Ngoma Hii

Msanii Nay wa Mitego ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Saka hela’ ameonyesha wasiwasi na kuhofia wimbo wake mpya ambao utatoka siku ya Jumatatu ya tarehe 11 kufungiwa.

nay wa mitego23

Nay wa Mitego amesema wimbo huo ‘Pale kati patamu’ anaamini utachafua hali ya hewa tena kwa mashabiki kutokana na kile alichokiimba ndani ya wimbo huo, kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego alisema kuwa akisikiliza wimbo huo yeye mwenyewe anapagawa yaani, na kuwataka mashabiki kushika hiyo tarehe kwani watathibitisha wenyewe.

“Zimebaki siku kadhaa tu, Jumatatu Tarehe 11. Nitakua naachi wimbo wangu mpya. ‘Pale kati Patamu’ hii ngoma daaah mpaka napagawa yani. Shika iyo Tarehe na siku pale kati patamu sijui wataleta zengwe na hii?” aliuliza Nay wa Mitego

Nay wa Mitego kabla ya kuachia wimbo wake wa Saka hela, alitoa wimbo uliokuwa unafahamika kama ‘Shika adabu yako’ ambao ulifungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364