-->

Alikiba Afungukia Ishu Yake na Hakeem 5

King wa bongo fleva Ali Kiba amesema kwa sasa hawezi kufanya kazi na Hakeem 5 hata kama ikitokea akiomba kolabo kwa kuwa uongozi wake ndiyo utatoa maamuzi ya nani kufanya kolabo na yeye kwa sasa.

kiba844

Hata hivyo Kiba amesema hana tatizo na Hakeem 5 kwani ni ndugu yake na anajua yote yametokea kwa kuwa kamsaidia Abby Skills ila Hakeem 5 anapaswa aelewe kwamba walisha saidiana kipindi cha nyuma na kwa sasa ana uongozi ambao ndo una pitisha kolabo zote anazotakiwa kufanya.

Pia Kiba alimalizia kwa kusema Abby Skills kwa sasa ni msanii wake na hakuamua kumchukua peke yake bali walikubaliana kama ndugu akiwemo Mr. Blue,Abby Skills na Hakeem 5 akiwemo kwa kuwa ni ndugu japo kitabia wanatofautiana.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364