Sina ‘Bifu’ na Bella – Chaz Baba
Mkongwe wa muziki wa dance nchini Chaz Baba amesena hana bifu lolote na msanii mwenzake Christian Bella na kwamba yeye ni ‘Team Bella’ damu.
Pia Chaz Baba amesema ni wakati tu haujafikia na muda ukifikia watakutana na Bella kwa kuwa tangu Bella anaingia Tanzania alikuwa anamuelewa na sasa anafanya vizuri katika muziki na mashabiki wake ndo mashabiki waliokuwa wanamshabikia yeye pia.
Hata hivyo Chaz amesema kwa sasa yeye anafanya kazi zake binafsi na kama kuna bendi ambayo inamtaka inatakiwa ikalipe baadhi ya madeni aliyokuwa anadaiwa na Mashujaa Band japo hana tatizo na uongozi wa bendi hiyo.
eatv.tv