Alikiba anena Seduce Me kushindanishwa na Zilipendwa, ‘Sijafuatilia wala siwezi’
Wakati ngoma ya Alikiba Seduce Me imetoka ilikuwa ikipanishwa na ile ya Diamond/WCB ‘Zilipendwa’ hasa katika mtandao ya Youtube, lakini Alikiba amefunguka na kusema hakuwahi kufuatilia hilo kabisa.
Wakati ngoma ya Alikiba Seduce Me imetoka ilikuwa ikipanishwa na ile ya Diamond/WCB ‘Zilipendwa’ hasa katika mtandao ya Youtube, lakini Alikiba amefunguka na kusema hakuwahi kufuatilia hilo kabisa.
“Sijafuatilia hiyo, na wala siwezi kufuatilia, mimi nilikuwa naangalia Saduce Me watu wanatuma screen shoot katika instagram, muda mwingine naangalia viewers wamefika wangapi, that’s it, sikuweza kuangalia wimbo mwingine wowote,” Alikiba ameiambia Bongo5.
Hadi sasa ngoma hizo katika mtandao wa YouTube zina views zaidi ya milioni 5, Seduce Me ikiwa na views milioni 5.8 na Zilipendwa views milioni 5.9.
Bongo5