-->

Nilikuwa Kama ‘Demu’ – Hemedi Phd

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hemed Phd amesema wakati anakuwa alikuwa mzuri kama mtoto wa kike, kitendo ambacho kilimuingiza kwenye matatizo mengi ikiwemo kufukuzwa shule.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Hemedi amesema muonekano wake wenye kuvutia, ulisababisha awe na mahusiano na mke wa mwalimu na kupelekea kufukuzwa shule aliyokuwa akisoma.

“Unajua kabla sijaanza kukua na kutoka zile chunusi chunusi mi nilikuwa kama demu, nilikuwa nahenyesha sana walimu wa kike walikuwa wananikubali sana, bebe zilikuwa zinaelewa sana, lakini kutokana na umri na mazingira nikawa navunga, nishapata kesi mimi nikiwa sekondari kidato cha pili  kutembea na mke wa mwalimu nikafukuzwa shule, lakini yote ni sehemu ya maisha tunapita”, amesema Hemedi.

Hemedi kwa sasa anadai mambo hayo ameacha kwa sababu ameshakuwa mtu mzima na yuko na familia, ambapo ana mke na mtoto mmoja. Lakini pia msanii huyo ameichia kazi yake mpya sasa inayojulikana kwa jila la ‘Mkimbie’.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364