-->

Alikiba Ashambuliwa na Mashabiki Kisa Lulu

KATIKA kile kilichoonekana kwamba amemkumbuka aliyewahi kuwa mpenzi wake zamani ambaye kwa sasa anatumikia kifungo gerezani, Elizabeth Michael ‘Lulu’, staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba hivi karibuni alishindwakuficha hisia zake na kuweka picha ya mrembo huyo ambapo baadhi ya mashabiki walimshambulia huku wengine wakimpongeza.

Kiba aliweka picha hiyo ya Lulu kwenye ukurasa wake wa Instagram bila kuandika kitu chochote na kupata mashabiki wengi ambao walianza kuchangia huku wengine wakimnanga kwamba huenda anatafuta kiki na wengine wao wakionesha kusikitishwa na Lulu kuwa gerezani. “Sisi tunataka kazi mpya hatutaki mambo haya, au ni kiki! Kama ni Lulu basi tunaomba mtuletee picha mpya za alivyo sasa huko gerezani jamani,” yalisomeka baadhi ya maoni.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364