Alikiba Atoa Madai Haya Kuhusu Tamasha la Mombasa Rocks
Hatimaye Alikiba ameeleza sababu ya kukatizwa kwa show yake kwenye tamasha la Mombasa Rocks ambalo Chris Brown pia alitumbuiza.
Kwenye tamasha hilo, Kiba alitumbuiza nyimbo mbili tu kabla ya mic aliyokuwa anaitumia kuonekana kupata mushkeli/kuzimwa na kumlazimu kuondoka jukwaani.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya, Willy Tuva akiwa bado Mombasa, Alikiba amedai kuhusi kufanyiwa hujuma.
“Kila mtu alikuwa na agreement yake. Mkataba wa Chris Brown unasemekana ni kwamba alikuwa anataka kuondoka muda mchache na dakika alizokuwa amepewa ni 80,” amesema hitmaker huyo wa Aje.
“So na time ndio ilikuwa inaondoka na ndege yake ilikuwa akimaliza kuperform ilikuwa inaanza kuondoka. Sasa sikujua ni kitu gani ambacho kimefanya mpaka mtu amekuja pale amedisconnect mic na nini. Halafu kuna vitu ambavyo sijavielewa ambavyo vilikuwepo pale, mimi pia sijafurahishwa navyo,” amesisitiza.
“Nilimuona meneja wake Diamond alikuwepo pale, anafuata nini backstage wakati mimi naperform, yeye anahusika kama nani? Haileti picha nzuri. Kwasababu hata kama watu wanafikiria kwamba of course hatuna beef lakini sasa umefuata nini na vitu kama hivyo vinahappen, wewe unafikiria watu watafikiria nini? Kitu gani kimemfanya aje? Kuna watu wengi waliokaa kwenye VIP unaweza ukaangalia show, kuja kwenye show, kaa kwenye VIP, angalia show. But alikuwa anafanya nini backstage wakati mimi naperform?” amehoji msanii huyo.
Hata hivyo anasema hawezi kumfikiria moja kwa moja kuwa meneja huyo wa Diamond alihusika kwenye tukio hilo, japo hakuubariki uwepo wake nyuma ya jukwaa la tamasha hilo.
“Sijajua mic imekatwa kwasababu Chris Brown alitakiwa kupanda au ni nini lakini nimekuwa surprised kwasababu unajua niko na fanbase kuwa na watu walikuwa wanaexpect hata before sijapanda walikuwa wanataka mimi niperform, wananiita ‘Ali Ali, vipi unakuwaje.’ Nikaingia, sijamaliza kuperform wamekataa mic, I think wameelewa kitu gani kinaendelea sababu it was not my fault.”
Hata hivyo Alikiba anasema alifurahi kurejea tena kutumbuiza japo haikuwa live kama alivyokuwa anafanya mwanzo.
Bongo5