-->

Amber Lulu Afungukia Kukamatwa na Unga

Kufuatia madai ya kukamatwa akisafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ jijini Arusha kuelekea China, video queen matata Bongo, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ amefungukia ishu hiyo akidai kuwa anaamini ilitengenezwa na watu walioamua kumchafua.

amber-lulu

Lulu Auggen ‘Amber Lulu’

Amber Lulu aliliambia Wikienda kuwa alishangaa kuona mitandaoni kwamba amekamatwa na unga, lakini hakuna kitu kama hicho kwani hajawahi kukamatwa.

Kabla ya kumpata Amber Lulu, simu yake ilikuwa haipatikani hivyo Wikienda lilimtafuta mdogo wake aliyeko jijini Mbeya ambaye naye alikiri kutompata mrembo huyo hewani kwa siku tatu ambapo ndugu walimtafuta kwenye vituo vya polisi jijini Arusha bila mafanikio.

Wapo baadhi ya watu waliodai kuwa ni kiki iliyofanywa na Amber Lulu mwenyewe ili kuwafanya watu wamuongelee.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364