Alikiba Awapa Neno Mashabiki
Msanii Alikiba ambaye sasa anatamba na ngoma yake mpya ‘Seduce me’ amefunguka na kuwapa neno la pongezi mashabiki zake baada ya kuiwezesha ngoma yake hiyo mpya kufikisha watazamaji zaidi ya milioni nne ndani ya siku 10.
Alikiba ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwashakuru mashabiki zake na kuendelea kuifanya ngoma hiyo kushika nafasi ya kwanza katika video ambazo zinafanya vizuri Tanzania toka ilipotoka Agosti 25, 2017 na kushuka kwa nafasi moja kwa masaa kadha na baadaye kurejea katika nafasi ya kwanza mpaka sasa.
“Seduce Me imefikisha watazamaji milioni 4 ndani ya siku 10 na bado inaendelea kushika nafasi ya kwanza kwa video zinazo ‘trend’ Tanzania, nawakubali wote na kuwathamini lakini pia nawapenda sana Tanzania” aliandika Alikiba