-->

Kajala: Sina Mpango wa Kuolewa Tena

UKITAKA kutaja majina ya mastaa wakali katika kiwanda cha Bongo Muvi, huwezi kuacha jina la muigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ ambaye ni mmoja wa wanawake wakali wa tasnia hiyo.

Kajala ambaye ni mama wa mtoto mmoja ana historia kubwa mpaka hapo alipo hivi sasa na ukitaka kujua mengi fuatilia katika makala hii kama ifuatavyo.
Over Ze Weekend: Kajala mwanao Paula amekuwa msichana mkubwa unapambana naye vipi ili kuhakikisha anaepukana na vishawishi?

Kajala: Kwanza kabisa nafikiri watu hawaelewi mimi ni mama wa tofauti kabisa ni mkali sana lakini najaribu mno kuzungumza naye kama rafiki.
Over Ze Weekend: Unasema wewe mkali lakini anapokuona unatoka usiku au kuvaa mavazi tofauti huoni hapo inamchochea zaidi?

Kajala: Hapana nafikiri kwanza hakuna kitu ambacho kitakuwa ni kigeni kwake hata kama atakuja kuwa mkubwa zaidi ya alivyo na kila siku namfundisha ajaribu kukua na tabia yake yeye.

Over Ze Weekend: Mashabiki wanajua ulishaolewa, vipi una mpango wa kurudi kwenye ndoa yako au una mpango wa kuolewa na mtu mwingine.
Kajala: Hapana sina mpango wa kurudi tena kwenye ndoa yangu wala kuolewa tena.
Over Ze Weekend: Kwa nini na wakati mumeo alipopata matatizo mpaka kwenda jela mlikuwa hamjaachana?

Kajala: Kuna mambo mengi sana yamepita ndiyo maana na pia sipendi kuyaelezea.
Over Ze Weekend: Kuna manenomaneno mara nyingi ukiwa na mwanaume anapata mabalaa kama mwenye hela anafilisika, vipi unazungumziaje hiyo?
Kajala: Mmh! Sasa hayo maneno hata wewe utayaamini kweli maana hivyo vitu vinatokea wala si kwamba nina gundu.

Over Ze Weekend: Kwa nini ugomvi wako na Wema hauishi?
Kajala: Mimi sina tatizo kabisa na mara nyingi ninapenda kama kuna tatizo liishe, lakini naona mwezangu bado moyo wake hajaufungua.

Over Ze Weekend: Kuna madai kuwa mara nyingi wewe unapenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na vijana ambao umewapita umri, unalizungumziaje hilo?
Kajala: Hiyo kali jamani mimi sidhani, hao wanaosema hivyo wananielewa mimi vilivyo, kama kuwa na uhusiano na mtu inatokea tu jamani.

Over Ze Weekend: Mastaa wengi wamekuwa wakijibweteka
kutegemea hela za mapedeshee unazungumziaje hilo?
Kajala: Sidhani kama hilo lipo kwa hivi sasa kwa kuwa kila mtu anatafuta maisha, hakuna wa kumuhonga mwenzake.

Over Ze Weekend: Umeshawahi kuhongwa mara ngapi?
Kajala: Si unajua mimi ni mwanamke ni mara nyingi tu inatokea.
Over Ze Weekend: Tangu uanze kazi ya uigizaji nini umefaidika kupitia kazi hiyo.
Kajala: Faida zipo, lakini si kihivyo kutokana na kazi zetu hizi za filamu zilivyo.
Over Ze Weekend: Ulishawahi kujaribu kuvuta unga?
Kajala: Hapana, ila bangi huko nyuma niliwahi kujaribu.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364