-->

Alikiba Kujaza ‘Wa Kimataifa’ Kwenye Albam Yake

Msanii Alikiba ameingia katika orodha ya miongoni mwa wasanii wanaotarajia kufanya mapinduzi ya muziki kwa mashabiki zao kwa kutoa albam.

Baada ya kutua katika Jiji la Dar es Salaam akitokea nchini Afrika Kusini siku ya jana, ‘King’ Kiba aliwashukuru mashabiki zake kwa upendo walioonesha kwake kwa kumsubiria muda mrefu bila ya kukata tamaa na kusema endapo mambo yakienda vizuri na yaye anatarajia kuachia albam ambayo atafanya na wasanii wa kimataifa bila ya kuwasahau hapa bongo.

“Chochote kinaweza kutokea ila kwa sasa hivi niko ‘busy’ namalizia albam yangu mpya itakuwa na vichwa ‘international’ na ‘local’ itakuwa ‘full’ nadhani itatoka mwaka huu kama mambo yakiwa fresh Inshaallah Mungu asaidie”. Alisema Kiba

Vilevile msanii huyo amesema amefurahi na ameipenda sana zawadi aliyopatiwa na rapa chipukizi Harmorapa wakati amekwenda kumpokea katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.

 Eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364