-->

Jike Shupa Aununua Ugomvi wa Batuli, Wema!

VIDEO Queen Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ ameibuka na kudai kuwa, hawezi kumuacha shoga yake Wema Sepetu ashambuliwe halafu yeye abaki kimya kwani anaamini anayoyafanya yuko sahihi hivyo anatangaza kuununua ugomvi.

Jike Shupa akiwa na Wema

Jike Shupa aliyasema hayo juzikati baada ya kuibuka kundi la wasanii wa Bongo Muvi na kumshambulia Wema baada ya kujiunga Chadema ambapo inadaiwa sasa hivi kuna bifu kubwa kati ya Yobnesh Yusuf ‘Batuli na Wema.

“Kwanza kwa wasiojua na mimi nipo Chadema, sasa hao akina Batuli wanaoibuka na kumchamba Wema, nitakula nao sahani moja.

Ninachoamini yeye alikuwa na uhuru wa kufanya na kuongea kile alichojisikia na hao wanaompaka matope wajue nimenunua huu ugomvi kwa buku kumi tu,” alisema Jike Shupa. Jike Shupa katika siku za hivi karibuni ameonekana kuwa na ushosti na Wema lakini wafuatiliaji wa maisha ya mastaa wamemtahadharisha kuwa makini kwani staa huyo si mtu wa kudumu na marafiki.

Chanzo:GPL


 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364