Alikiba na Barakah Da Prince Wavamiwa na Watu 6 Afrika Kusini
Alikiba na Barakah Da Prince wamevamiwa na majambazi jijini Johannesburg, Afrika Kusini Alhamis hii.
Wawili hao waliwasili nchini humo asubuhi ya jana walikoenda kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kushoot video zao.
“Wote Alikiba na Barakah the Prince walikuwa pamoja na timu kwaajili ya mkutano wa utayarishaji kwenye ofisi zilizopo maeneo ya katikati za kampuni maarufu ya Afrika Kusini wanayofanya nayo kazi,” yamesema maelezo rasmi kutoka uongozi wa Rockstar4000.
“Wakati wakiendelea na mkutano, watu sita waliokuwa na bunduki walivunja kuta za jengo la ofisi hiyo na kuingia walipokuwa Alikiba, Barakah The Prince na wengine,” yamesema.
“Watu hao wakiwa na bunduki zao waliwapora mali zao na vitu vingine vilivyokuwemo ofisini humo. Hata hivyo tunafurahi kuripoti kuwa si Alikiba, Barakah The Prince wala timu imejeruhiwa kwa namna yoyote ile,” yamesisitiza maelezo hayo.
“Wote Alikiba na Barakah The Prince wanapenda kuwahakikisha mashabiki wao kuwa wako salama na wanapumzika kwa siku moja kusahau tukio hilo baya lakini wamenuia kuendelea na miradi yao na hawatazuia kutoa miradi yao ijayo iliyopangwa kwaajili ya mashabiki wao Afrika na duniani kote.”
“Alikiba na Barakah The Prince wamepanga kuendelea na miradi yao iliyopangwa kufanyika Afrika Kusini hadi itakapokamilika.”
Barakah amemshirikisha Alikiba kwenye wimbo wake, Nisamehe na jana walipost video akiwa na muongozaji wa video, Meji Alabi.
Bongo5