-->

Muhogo Mchungu Afungukia Matumizi ya Kiswahili Kwenye Kazi za Sanaa

MKONGWE wa filamu nchini, Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’, amewataka wasanii wa Tanzania watumie lugha ya Kiswahili katika kazi zao badala ya kutumia lugha ya Kiingereza ili waikuze lugha hiyo

muhogo

Mwigizaji huyo alisema hayo juzi alipotembelea Ofisi za Kampuni ya New Habari (2006) Ltd wazalishaji wa magazeti ya Bingwa, Rai, Dimba na Mtanzania zilizopo Sinza Kijiweni jijini Dar es Salaam.

“Kazi zetu zinaangaliwa dunia nzima na sisi wasanii ndio tunatakiwa kuwa mstari wa kwanza kusaidia kuikuza lugha yetu kama tunataka nyumba bora ni lazima tuanze na msingi bora, ili lugha ya Kiswahili izidi kusonga mbele tunatakiwa kuitumia zaidi katika kazi na kuacha kutumia lugha za kigeni,” alisema mwigizaji huyo anayetarajia kucheza katika filamu mpya ya ‘Masomo’ pamoja na waigizaji wakongwe, Mzee Majuto na Mzee Korongo.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364