-->

Alikiba na Diamond Mjipange – Abdukiba

Msanii Abdukiba ambaye ni mdogo wa Alikiba amefunguka na kutoa ushauri kwa wasanii Alikiba na Diamond Platnumz kuwa wanapaswa kujipanga kimuziki na katika kazi zao kwani kuna vijana wengi wanajipanga kuchukua nafasi zao.


Abdukiba alisema hayo kupitia kipindi cha ‘Ngaz kwa ngaz’ kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana EATV, Abdukiba anasema wapo wasanii wengi wadogo wanajipanga kuona wasanii hao wanatoka kwenye nafasi zao hizo, ambazo zinawapa ushindani na hamasa kikazi.
“Lakini Diamond na Alikiba waamini kwamba wapo watu wanajipanga kuweza kuwatoa kwenye nafasi zao, wapo wengi ambao wanaweza kufanya hivyo nadhani bado hawajafikia muda” alisisitiza Abdukiba

eatv.tv

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364