-->

Serikali Yatetea Ada za Uhakiki wa Filamu

Serikali imetetea ada za uhakiki wa filamu zinazotozwa hapa nchini na kusema kuwa ada hizo zipo kwa mujibu wa sheria na kanuni, huku ikifafanua kuhusu utaratibu wa kulipwa kwa ada hizo.

Mh. Anastazia Wambura

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Anastazia Wambura ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi juu ya Serikali ina mpango gani wa kuwapunguzia wasanii gharama za ukaguzi ambapo kwa hivi sasa gharama hizo ni shilingi elfu moja kwa dakika.

“Nchi yetu hutoza ada ambazo ni rafiki ukilinganisha na nchi nyingine, kwa mfano, Nigeria ambayo ni nchi iliyopiga hatua kubwa kwa upande wa filamu, hutoza filamu yenye urefu wa dakika 60 (filamu ya lugha asili) Naira 30,000 sawa na zaidi ya dola 150 ambayo ni sawa na Sh. 337,950 za Kitanzania na Kenya, ni sawa na Sh. 190,000,” alifafanua Anastazia Wambura.

Aliendelea kwa kusema kuwa Tanzania hutoza filamu za Kitanzania zenye urefu wa dakika 60 kwa Sh. 60,000 (sawa na Sh. 1,000 kwa dakika) ambapo gharama hizo ni sawa na asilimia 18 ya gharama za Nigeria na asilimia 32 ya Kenya.

Amesema kwa gharama hzo, ni wazi kuwa Tanzania imekuwa ikitoza ada hiyo ya uhakiki wa filamu kwa gharama nafuu na rafiki ukilinganisha na nchi nyingine Afrika

eat.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364