Alikiba na Diamond Wananiumiza Sana Kichwa – Z Anto
Msanii wa muziki aliyewahi kufanya vizuri na wimbo Binti Kiziwi, Z Anto amesema siku yoyote kuanzia sasa anaachia ngoma yake mpya na video huku akidai watu anaowawaza na kuwafikiria sana kuwa ni Alikiba, Diamond Platnum pamoja na Vanessa Mdee.
Z Anto ameiambia Enewz ya EATV kuwa ujio wake mpya katika muziki wa bongo fleva unakuja kuleta heshima tena ya muziki huo na kusema kipindi yupo kimya alikuwa anajifunza mengi kupitia wasanii wa sasa na kusema ameona mapungufu yao hivyo yeye anakuja kuwafundisha sababu tayari amewasoma na kufanya kitu kupitia makosa yao hivyo watajifunza kupitia yeye.
“Kuna wasanii wengi wanafanya vizuri lakini ambao naweza kusema wanaoangaliwa na wengi ni Diamond na Alikiba pamoja na Vanessa, hawa ukitaka kwenda mbali zaidi au kimataifa unatakiwa kushindana nao na ndio kitu ambacho nakiandaa,”
Muimbaji huyo amedai ukimya wake kwenye game, umeutumia kuisoma tasnia ya muziki ili akirudi asimuache mtu.