-->

Wapinzani Watapotea – Mrisho Gambo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kusema kuwa wapinzani wa Tanzania kama hawatabadili aina ya siasa wanazozifanya sasa basi watapotea kwani serikali ya awamu ya tano imepata Rais ambaye hataniwi na wala hatishiki.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

Gambo amesema kuwa wapinzani baadala ya kuanza kupiga porojo zisizo na msingi bali wajipange tu kumsaidia Rais John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano.

“Nataka niwaambie wanasiasa hawa wa upinzani wasipobadilisha aina ya siasa wanayofanya kwa ninavyoiona mimi serikali ya awamu ya tano watapotea, kwa sababu tumepata Rais ambaye hatanii, unajua wameshazoea wengine wakitishwa tishwa kidogo wanaingia mitini huyu Magufuli akinyooka amenyooka, ananyoosha rula tu utaamua mwenyewe ukae kushoto au kulia. Kwa hiyo mimi niwashauri tu itakuwa vizuri badala ya kupiga porojo wajipange kumsaidia Rais aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano” alisema Gambo

Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa huyo wa Arusha amesema kuwa kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kutaka kuikwamishan serikali basi watadili naye asubuhi mchana na jioni.

“Kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kuikwamisha serikali isitekeleze malengo yake nataka niwahakikishie kwa uwepo wangu hapa tutahangaika naye asubuhi, mchana na usiku kwa mbinu zote zile, kama wanataka porojo wasubiri 2020, sasa hivi kama wanataka tusaidiane kupeleka huduma na maendeleo kwa watu, haiwezekani tukawa na serikali au nchi ambayo kila siku ni porojo tu, kila siku siasa” alisisitiza Mrisho Gambo

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364