-->

Alikiba: Sipendi Kiki na Sitofanya Kamwe

Mkali wa Bongo Fleva Alikiba amesema Kiki ni kitu ambacho hakipo kwenye menu yake.

ali-kiba90

Alikuwa akiongea kwenye kipindi cha Clouds 30 kupitia Clouds TV.

Kwanza kwangu mimi hicho kitu hakipo, sijui kusema mimi nina hela. Na kuna watu wengine wanaongopa kwa kusema uongo tu kwasababu watanzania tumeshakubali kupelekwa na hiyo,” alisema.

“Lakini kuna baadhi pia ya watanzania wapo makini sana, huwa hawakubali kitu kirahisi na kuna wengine ni wepesi sana kuamini. Na hizi kiki zinakuja kwasababu watu wanaamini. Mimi binafsi sitaki kabisa hivyo vitu na sitokuja kufanya na kama kuna watu wanafanya hivyo vitu mimo nimewaambia unajua kila mtu ana identity yake kwamba hawa ni watu wa aina hii na hawa ni hii.”

Ukiongea kitu mtu mwenye akili zake timamu anajua kabisa hii si kweli na Alikiba hawezi kufanya hivyo. Ila huyu anaweza kufanya hivyo na huyu hawezi kufanya hivyo ila Alikiba anaweza fanya hivyo,” alisisitiza.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364