-->

Tuzo Zitaongeza Thamani ya Mauzo ya Filamu- Rais wa TAFF

Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifwamba amesema tuzo ambazo zimeandaliwa na EATV ambazo zipo kwenye mchakato sasa na wasanii mbalimbali wamejitokeza kujipendekeza katika tuzo hizo zitasaidia wasanii kupaa katika mauzo ya kazi zao.

Simon Mwakifwamba

Simon Mwakifwamba

Mwakifwamba ameyasema hayo alipokuwa akiongea na EATV akitoa mtazamo wake kuhusu kuanzishwa tuzo hizo na faida ambazo msanii anaweza kuzipata kwa kushiriki kuwania tuzo hizo.

“EATV AWARDS zitasaidia sana kuongeza thamani ya mauzo ya wasanii kwa kuwa hata watu wanaotaka kununua kazi ili ziende sokoni watamtazama msanii kwamba ni mtu mkubwa kutokana na kwamba ameshinda tuzo za EATV AWARDS” Amesema Mwakifwamba

Mwakifwamba ameongeza kuwa kila mshiriki ambaye atachaguliwa katika tuzo hizo tayari ni mshindi na kuwataka wasanii kuchangamkia fursa kama hizo pindi zinapojitokeza kwa sababu zitasaidia kuinua kazi zao za sanaa.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364