-->

Amini Afungukia Kutompongeza Linah

Msanii wa Bongo Flava, Amini amefunguka mambo kadhaa kuhusu aliyekuwa mpenzi wake Linah tangu alipojifungua.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Yamoyoni’, ameiambia XXL ya Clouds Fm aliposikia Linah amejifungua alimuombea tu ila hakuweza kumpatia zawadi yoyote.

“Sikuwahi kumpongeza wala kumpelekea zawadi kwa sababu sifahamu anapokaa, vile vile sina mawasiliano naye. Niliposikia amejifungua mtoto wa kike nikasema Mwenyenzi Mungu amfanyie wepesi na mtoto wake na waweze kuishi vizuri katika maisha yao,” amesema.

“Yeye hakuwahi kunikosea hata mimi sikuwahi kumkosea kwa hiyo sikuwa na sababu ya kusema kitu gani bwana, ila kimoyomoyo nilimuombea dua kwa sababu alikuwa anahitaji sana mtoto,” ameongeza.

Wawili hao ambao muziki wao ulitambulika kupitia THT walikuwa mapenzini kipindi cha nyuma kabla ya kila mmoja kuanza maisha mapya ya kimahusiano.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364