-->

Dogo Janja Amfungukia Irene Uwoya, ‘Nampenda Sana’

Msanii wa Bongo Flava, Dogo Janja amezungumzia taarifa zilizokuwa zikidai kuwa anatoka kimapenzi na Muigizaji wa filamu Irene Uwoya.

Rapper huyo ambaye ameachia ngoma mpya leo ‘Ngarenaro’ amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa ukaribu wao ulikuwa wa kawaida tu na hakuna kilichokuwa kinaendelea kati yao ingawa watu waliwachukulia vinginevyo.

“Nampenda sana yule dada lakini kuwa na mazoea naye kidogo kumezua maneno mengi,” amesema Dogo Janja.

July mwaka huu zilienea taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wameonakana jijini Mwanza katika matanuzi  ya nguvu kitu kilichozua minong’ono kuwa wapo mapenzini.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364