Aunt Ajinasua kwa JPM
Hatimaye staa wa Bongo Muvi, Aunt Ezekiel Grayson amefanya kila liwezekanalo na kujinasua mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Pombe Magufuli ‘JPM’ kwa kukomboa gari lake aina ya Audi lililokuwa limeshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kushindwa kulipa kodi.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa mbwembwe kibao wikiendi iliyopita, Aunt alimshukuru Mungu kwa kumnasua kwenye soo hilo kwani alikuwa akiishi kwenye lindi la mawazo kwa zaidi ya wiki tatu tangu gari hilo likamatwe.
“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kutoa shilingi milioni 15 na hatimaye nimekomboa gari langu ambalo lilikuwa kwenye hatihati ya kupigwa mnada na TRA,” alisema Aunt.
Chanzo: GPL