-->

Aunt Ezekiel Afunguka Sababu ya Kutamani Kujifungua Mtoto wa Kike Tena

Msanii wa filamu nchini Aunt Ezekiel amedai kuwa anatamani tena ajifungue mtoto wa kike kwa mara ya pili kwani watoto wa kike kuwa nao ni pesa.

Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live Aunt Ezekiel aliweka wazi kuwa watoto wa kike ni pesa ingawa hakutoa ufafanuzi ni pesa kwa namna gani lakini anasema anatamani ajifungue tena mtoto wa kike.

“I wish nipate mtoto wa kike tena, watoto wa kike hela ile, yaani mpaka wajae” alisema Aunt Ezekiel

Mbali na hilo Aunt Ezekiel anakiri kuwa kwa wanaume wote aliokuwa nao hakupata kitu cha maana ila toka amekuwa na mzazi mwenzake ambaye ni Moze Iyobo anaona kuna mambo mengi ya maendeleo ambayo ameweza kufanya, hivyo Moze amembadilisha sana maisha na kumfanya apige hatua za maendeleo.

“Kuwa na Moze Iyobo kumenipeleka mbele sana kimaendeleo, kote nilikopita sijapata kitu cha maana” alisema Aunt Ezekiel kwenye Friday Night

 

 

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364