-->

Aunty Ezekiel Azipondea Filamu Alizocheza Zamani

Mrembo aliyekuwa kimya kwa muda mrefu katika uga wa Bongo Movie mwanadada Aunty Ezekiel amerudi kwa kishindo na kazi mpya ambayo imemfanya aziponde kazi zake za zamani kutokana na ubora wake.

Aunt Ezekiel akiwa na waigizaji wenzake, JB na Kajala

 

Aunty aliyekuwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV amesema movie ambayo amekuja nayo sasa ni ya viwango vya hali ya juu, na ina utofauti na movie zote alizowahi kucheza siku za nyuma kwa kuachana na mambo ambayo anadai kuwa hayakuwa na maana kwenye movie.

Movie hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Christmas Eve’ ambamo Aunty anatumia jina la Salome, inazinduliwa leo na itakuwa LIVE kupitia EATV kuanzia saa 3:00 usiku, ambapo Aunty pia ameeleza sababu za kuifanyia uzinduzi movie hiyo kuwa ni pamoja na kuwaonesha mashabiki wake utofauti wa movie hiyo na kazi zake zamani

“Tumefanya kitu tofauti, siyo kama ile ya zamani ya kwenye makochi, unaingia shikamoo baba, halafu mambo yanakuwa yaleyale, tumeona tuzindue kwa kishindo ili kuwaonesha watu utofauti” Amesema Aunty.

Katika hatua nyingine Aunty alikiri kuwa yeye ni mjamzito na kwamba hicho ni kitu ambacho hawezi kuficha wala hana sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa ujauzito haufichiki na pia kuweka wazi kuwa sasa amebadili mtindo wake wa maisha na kuachana na mambo aliyoyaita kuwa ni ya kitoto.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364