-->

AY Afunguka ya Moyoni Kuhusu Joh Makini

Msanii mkongwe katika ‘game’ la mziki wa kizaji kipya , Amwene Yesaya ‘AY’ amefunguka na kusema kuwa toka mwaka 2006 mpaka sasa hakuna rapa ambaye ameibuka na kuwa mkubwa zaidi ya Joh Makini.

AY amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kuanzia mwaka 2006 baada ya Joh Makini kuingia kwenye kundi la ‘A list’ ya rapa wazuri bongo hakuna rapa mwingine ambaye ameingia kwenye kundi hilo, ila amesema wapo rapa wamekuwa wakijitahidi lakini wanaishia ‘B, C na D list’ ya rapa wakali bongo.

“Toka mwaka 2006 hakuna rapa amekuwa mkubwa zaidi ya Joh Makini hapa bongo, wapo wanajitahidi lakini wengi wanaishia ‘B, C na D list’ hata Roma Mkatoliki ni rapa mzuri anajitahidi, lakini natoa ushauri tu kuwa rapa tunatakiwa kuongeza nguvu ya kujitangaza na kazi zetu, maana unaweza kuwa unaweza sana lakini bila kujitangaza huwezi kuonekana” alisema AY 

Mbali na hilo AY alitoa ushauri tena kwa wasanii wa hip hop Bongo na kuwataka kutengeneza brand zao na kazi zao kwa kutafuta ‘interview’ mbalimbali na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania ili kuongeza wigo wao na kutanua mipaka ya kazi zao.

“Unajua hata rafiki yangu Fid Q nilishawahi kumwambia hata kama wewe ni mkali na unajijua ni mkali sana kitu kikubwa unachohitaji ni kujitangaza , hivyo rapa tunahitaji kujitangaza sana na kutangaza kazi zetu, tujaribu kutafuta Interviews mbalimbali, nataka kuona rapa wetu mwaka 2017 wanashiriki matamasha makubwa, wajiongeze nina uhakika tutafanya makubwa zaidi” alisema AY 

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364