-->

Muigizaji Mtanzania Ateuliwa Kuwa Rais wa Kampuni ya Filamu kwa Trump

Muigizaji na mtayarishaji wa filamu kutoka nchini Tanzania, anayefahamika zaidi kupitia filamu ya Going Bongo, Ernest Napoleon (pichani hapo chini), ameteuliwa kusimamia kampuni ya Kimataifa ya utengenezaji na usambazaji filamu, D Street Media Group, kama Rais.

Kampuni hiyo yenye Makao Makuu yake katika nchi anayoiongoza Rais Donald Trump, Marekani kwenye jiji la New York na Ofisi Mjini Berlin, Cape Town na Buenos Aires, Napoleon atakuwa na cheo cha pili kwa ukubwa baada ya Mkurugenzo Mtendaji (CEO), Dexter Davis kwenye kampuni hiyo.

Moja ya majukumu ya Napoleon, atakuwa akisimamia zaidi kazi za kampuni hiyo upande wa Afrika na Mashariki ya Kati, japo hiyo haimaanishi kuwa hatohusika na masuala mengine ya kampuni hiyo duniani kote.

“Hii ni fursa ya kipekee katika hatua hii ya career yangu. D Street Media Group ni kampuni ya kujitegemea inayokua kwa kasi ikiwa imeshika kila upande wa dunia. Ni heshima kubwa kwangu kuendeleza biashara yetu katika masoko ya Afrika na Mashariki ya Kati ambayo nayaelewa vyema,” amesema Napoleon.

Aliendelea, “Naamini kuna fursa nyingi kwa kampuni ya Kimarekani kama D Street barani Afrika, na tukiwa na washirika sahihi kutengeneza maudhui mazuri, tutafanikiwa Afrika na hasa Marekani na nje ya nchi.”

Blues

Kwa upande wake, Davis alisema, “Ninafurahi kuleta mshirika mchangamfu kama Ernest, sifa zake kama muigizaji na mtayarishaji, kutamfanya awe rais mzuri. Kwa haraka amekuwa na jina Tanzania, sehemu aliyozaliwa baba yake na ambako amekulia. Nimesikia mambo ya kuvutia kuhusu Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, na ninafurahi kuwa na Ernest ndani yetu kutuongoza katika mafanikio ndani ya bara la Afrika,” alisema Davis.

“Kuhusu ukweli kuwa Ernest anazungumza Kiswahili, Kirusi, Kiswidishi na Kiingereza, ni asset pia. Ongeza hapo ukweli kuwa ni mtayarishaji anayetaka kuileta Afrika na Waafrika kwenye jukwaa la dunia ni kitu ambacho kimenifurahisha na kujivunia zaidi.”

D Street tayari ina uwepo wake barani Afrika ikiwa na ofisi Cape Town, Afrika Kusini. D Street Pictures, tawi la utayarishaji, lilitayarisha filamu ya Afrika Kusini, iitwayo ‘Musiek vir die Agtergrond,’ filamu ya Kiafrikaan iliyowekeza mwaka 2013.

Kampuni sasa ipo kwenye utayarishaji wa mwanzo wa filamu iitwayo ‘The Blue Mauritius.’ Muingozaji wa Uingereza, Charles Henri Belleville, (Jet Trash, The Inheritance) ataiongoza. Belleville amemaliza kuongoza filamu yake ya pili na mtajwa wa tuzo za Oscar, Tom Hardy (Mad Max, Legend).

Kisa cha filamu ya ‘The Blue Mauritius’ kinawahusu wezi watano wa kimataifa wanaoenda Cape Town kuiba muhuri wenye thamani zaidi duniani. Filamu hiyo imekusanya mastaa duniani akiwemo muigizaji wa Marekani, Eric Dane (Grey’s Anatomy, Last Ship), Brian Cox (The Rise of the Planet of the Apes, The Bourne Supremacy), John Ryes-Davies (The Lord of the Rings, Raiders of the Lost Ark) nguli wa Ufaransa, Gerard Depardieu (Life of Pi, The Man in the Iron Mask), kutaja wachache tu.

‘The Blue Mauritius’ itatengenezwa Cape Town na katika mji mdogo wa pwani, Port Shepstone, Afrika Kusini. Ni filamu iliyolenga soko la kimataifa lakini yenye kisa cha Kiafrika. Mastaa wa Afrika Kusini akiwemo Pearl Thusi na Lwandle Ngwenya, nao watashiriki.

Hiyo ni sehemu ya harakati za D Street kuendeleza na kutayarisha filamu za biashara za Kiafrika zitakazosafiri dunia nzima na kutengeneza mastaa wa Kiafrika. Ikiwa na kampuni ya utayarishaji na usambazaji yenye makazi yake Marekani, inafanya hili liwezekane zaidi. Filamu hiyo inatayarishwa na Davis pamoja na rapper, muigizaji na mtangazaji wa Marekani, Nick Cannon (Chi-Raq, America’s Got Talent).

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364