AY Atoboa Haya Usiyoyajua Kuhusu P-Funk
Ambwene Yessaya aka AY amefunguka kwa kumtaja mtayarishaji wa muziki mkongwe hapa Bongo, P-Funk Majani ndiye alimpatia majina yake mawili ya utani.
Rapper huyo ameyataja majina aliyopewa na mtayarishaji huyo mkongwe ni pamoja na jina la Mzee wa Commercial ambalo alipewa mwaka 2001 na El Chapo ilikuwa mwaka 2012.
Kupitia mtandao wake wa Instagram, AY ameandika:
Was a great moment kumeet na GodFather wa Bongoflava @majani187 ndio aliyenipa wazo la kufanya muziki kama SOLO ARTIST na kunipa nafasi ya kurecord kwenye studio yake #BONGORECORDS 2001 wimbo wangu wa kwanza kama AY #NiRahaTu ..Aliyenibatiza a.k.a ya MZEE WA COMMERCIAL (2001) na EL CHAPO (2012) ..God Bless you Bro..Soon Nibless na Production yako nyingine ????
Bongo5