-->

JB Aongea Kuhusu Mfumo Huu Mpya wa Uzinduzi wa Filamu

Mcheza filamu maarufu Jacob stephen (JB) amefanya mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kutambulisha mfumo mpya wa kuonesha filamu kupitia media ya Sibuka Maisha channel 111 kwenye startimes kabla ya kuingia madukani.

jb92

Amesema filamu hiyo inaoneshwa kwa mara ya kwanza Ijumaa tarehe 23 mwezi huu saa 3 usiku na kurudiwa Jumamosi na Jumapili ili kuwapa muda mashabiki zake waweze kuona filamu hiyo

Aidha ameishukuru kampuni ya Steps entertainment kwa kuanzisha mfumo huu mpyaa wa kuonesha filamu kabla hazijaingia sokoni

Filamu hii inatarajia kuingia sokoni Jumatatu 26 mwezi wa 9 nchi nzima,kwa sasa hivi Jb anatamba sokoni na filamu ya chungu cha tatu akiwa na Wema Sepetu na wasanii wengine wengi.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364