-->

AY:Kurudi kwa ‘East Coast Team’ Kupo Mikononi Mwa King Crazy GK

Msanii AY ambaye ni miongoni mwa wanaounda kundi la East Coast Team, amemtupia msanii mwenzake GK zigo la kurudisha kundi hilo.

ay03

Akizungumza kwenye eNewz ya East Africa Televisio, AY amesema uwezekano wa kundi hilo kurudi upo lakini mwenye uamuzi wa mwisho ni King Crazy GK ambaye amemtaja kama Amiri Jeshi mkuu wa kundi hilo.

“Kwanza East Coast Team ipo, ni kwamba mimi na FA tulitoka kufanya kazi zetu binafsi, ila kufanya kazi sisi wote watatu itatokea lazima tuifanye, kwa hiyo ni upande wake (GK) kuamua kwa sababu yeye ndiyo Amiri Jeshi mkuu, East Coast ilikuwepo na ipo, siyo kwa vile AY na FA wametoka”, alisema AY.

Pia AY alizungumzia kitendo cha msanii huyo kurudi kwenye game kwa kuamua kuimba, na kusema kuwa amefanya vizuri kwenye kurudi kwake.

“Nimeona amefanya comeback ya kwake na amejitahidi kwa uwezo wake, ameswitch na yuko sawa, mimi na GK tunashirikiana katika njia tofauti tofauti nje ya muziki pia”, alisema AY.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364