-->

Siri ya Moyo Itawazima Wakongwe-Man Fizo

SALUM Saleh ‘Man Fizo’ mwigizaji na mtayarishaji wa filamu anatamba kwa kujinasifu kuwa toka aingie na kupenya katika soko la tasnia ya filamu Swahilihood kila siku anapanda alianza na filamu kubwa ya Nimekosea wapi? iliyosumbua wakongwe anasema sinema yake ya Siri ya Moyo atawazima wakongwe.

man-fizo

Mna Fizo mtayarishaji wa filamu ya Siri ya Moyo.

“Siri ya Moyo ni kazi ambayo nimerekodi kwa zaidi ya miezi miwili nashukru editing imeeenda poa sana maana nikiwa Zanzibar ilibidi niingie studio na wasanii wangu kupata sauti bora ni sinema kubwa,”

“Sitaki kurudi nyuma ndio maana filamu yangu ya Siri ya Moyo niliamua kwenda Zanzibar na kuitengezea Siri ya Moyo ni kazi kubwa sana na nimetuma baadhi ya scene kwa wadau wakubwa ananiogopa sasa,”alisema Man fizo.

Man Fizo anasema kuwa haikuwa rahisi sana kwani mara nyingi ilikuwa ili ukubalike na soko ni lazima ushikwe mkono na wasanii wenye majina lakini yeye alijitoa mhanga na kuanza kutengeneza filamu kwa kuwashirikisha wasanii wenye majina lakini huku yeye akiwa mhusika mkuu na kafanikiwa kuliteka soko hilo.

Katika filamu hiyo inakutanisha wasanii wenye uwezo mkubwa katika tasnia ya filamu Swahilihood kama vile Deus Mihambo, Mwanaheri Afcery, Salum Salehe ‘Man Fizo’ na wasanii wengine wakali Bongo.

man-fizo45

Mna Fizo mtayarishaji wa filamu ya Siri ya Moyo.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364