-->

Baada ya Harmonize, Rayvanny kufanya yake

Baada ya Harmonize na Rayvanny kusainiwa lebo ya WCB na kutumia studio ya Wasafi, kurekodia nyimbo zao sasa tutegemee kusikia sauti hizo katika studio zingine.

Kwa mujibu wa Diamond Platanumz akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, amesema kuwa Rayvanny, naye anatarajia kufungua studio yake ya muziki itakayo weza kutengeneza midundo chini ya mtaarishaji Rash Don aliyejiongezea umaarufu kutoka Kili Records.

“Kitu kingine ambacho watu hawakijui ni kuwa Rayvanny atafungua studio yake na producer wake atakuwa Rash Don,” amesema Diamond ambaye ameachia wimbo wake mpya ‘Fire’ aliomshirikisha Tiwa Savage.

Ray atakuwa msanii wa tatu chini ya lebo hiyo yenye wasanii sita mpaka sasa kuwa na studio yake, baada ya Diamond anayemiliki studio ya Wasafi na Harmonize ambaye naye anamiliki studio yake binafsi.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364