-->

Dogo Janja Aruka kwa Muna Love

Msanii wa hip hop Dogo Janja amekanusha tetesi za kujihusisha kimapenzi na muigizaji wa zamani na mfanyabiashara Muna Love kwa kusema hajawahi kuwa na mahusiano na habari hizo zinamuweka sehemu mbaya katika mahusiano lakini pia kifamilia.

Janjaro amelazimika kufunguka hayo baada ya tetesi kuenea muda mrefu kujihusisha na Mwanadada huyo huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kusema kwamba analelewa na mfanyabiashara huyo.

“Hakuna kitu kibaya kama utandawazi, yaani kila mtu ana simu na bando lake kwa hiyo akiamka asubuhi anajisikia kufanya  chochote au kutunga vitu kama hivyo lakini siyo kitu kizuri, maana yananiumiza mimi na familia yangu, Uongozi wangu lakini pia vinamuumiza mpenzi wangu kwa sababu tuna malengo makubwa hivyo haya yanapoendelea yanazidi kumuumiza au kumchanganya”, Dogo Janja alifunguka.

Aidha Janjaro ameongeza kwamba “Mimi siyo mtu wa kuonesha maisha yangu binafsi kwenye mitandao ndio maana hata mpenzi wangu sijawahi kumuweka mitandaoni, maisha yangu binafsi ni ya kwangu na siyo ya kila mtu hata huyo dada wa watu anaumizwa na hili na anafamilia pia kwa hioyo hizi habari zinazidi kumuweka pabaya.

Pamoja na hayo Dogo Janja amewataka watu kutoamini chochote kinachoanzishwa kwenye mitandao ya kijamii mpaka atakapozungumza mwenyewe

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364