Baada ya Tuzo za BET, Diamond Kuja Upya na P Square
Tuzo za BET zimefanyika mwishoni mwa wiki hii pande za Los Angeles, Marekani ambapo msanii Diamond Platnumz aliwakilisha Tanzania ambapo mshindi aliyekuwa akiwania tuzo moja na msanii Diamond na wengine kutoka barani Afrika alitoka nchini Afrika Kusini ambaye ni Black Coffee. Diamond amezungumza na Clouds Fm.
‘’Kila kitu kimekwenda fresh tuzo za Afrika zimetolewa ambapo mshindi amekuwa Black Coffee mshindi wa ‘Best International Act’ kutoka South Africa, kwa sisi ambao ni Waislam tuaambiwa kila kinachotokea lazima umshukuru Mwenyezi Mungu kwasababu kwa baya na zuri lote linatokea kwasababu ya kukamilisha mwisho mwema anaupanga yeye, tumeshinda tuzo nyingi sana ukiangalia kuanzia mwaka jana hadi mwaka huu, Tanzania ndio imekuwa nchi ambayo imeongoza kwa kushinda tuzo nyingi sana Afrika kwenye muziki so tunapomis moja tusilalamike, Mungu anakuwa anatutia chachu tukazane zaidi ili tushinde tuzo nyingi sana baadae so watu waendelee kupush,kusapoti na wategemee vitu vikubwa kwasababu wiki hii nitaachia ngoma zangu moja niliyofanya na P Square’’
cloudsfm