Esha Atoa Sababu za Ubonge
MWIGIZAJI wa Bongo Muvi, Esha Buheti amedai kuwa ubonge alionao kwa sasa ni kwa sababu ya mapochopocho anayojipikia muda mwingi anapokuwa nyumbani na si kweli kwamba ni mjamzito kama watu wanavyomzushia.
Akizungumza na mtandao huu, Esha alifunguka kuwa, kila mtu anamshangaa kunenepa kwake lakini yeye hajutii kwani ni matokeo ya vyakula vinono na kwa mwezi huu mtukufu ndiyo hawezi kupungua kabisa.
“Mimi sina mimba, nimenenepa kwa kula tu, napenda kupika na kula vizuri hayo ndiyo mafanikio ndiyo maana nimenenepa,” alisema.
Chanzo:GPL