-->

Baba Levo ni Mazinguaji – Msechu

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Peter Msechu amefunguka na kusema kuwa kwa mtazamo wake, msanii Baba Levo ambaye kwa sasa ni Diwani, ni kati ya wasanii wazinguaji ambao wanatapatapa.

msechu933w

Peter Msechu alisema hayo kupitia kipindi cha ‘Ngaz kwa ngaz’ kinachorushwa na EATV ambapo alisema kwa kuwa Baba Levo ni msanii mzinguaji ndiyo maana ameamua kukimbilia kwenye siasa hivi sasa.

“Kwangu mimi msanii mzinguaji ni Baba Levo yule si msanii, huwezi kufanya show ina wabunge na waziri wewe unakwenda unapiga nyimbo za kihuni, mimi nafikiri staili ya baba Levo sidhani kama ni msanii anatapatapa ndiyo maana saizi amekimbilia kwenye siasa, kwangu mimi Peter Msechu show moja na Baba Levo sifanyi” alisema Peter Msechu

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364