-->

Bahati Adai Kuzinguliwa na Linex, Mwenyewe Akana

Msanii Bahati kutoka Kenya ameyafikisha mezani mambo yaliyotokea kati yake na Linex, mpaka kukosekana kwenye wimbo wake mpya wa ‘mapenzi’ ambao unafanya vizuri kwa sasa Afrika Mashariki.

linex

Bahati (Kushoto), Linex (Kulia)

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Bahati amesema walikubaliana na Linex na alisha rekodi sehemu yake na kwamba kilichobaki kilikuwa ni ku’shoot’ video ili kazi hiyo ikamilike, lakini Linex alikuja kumzingua na kumtosa mwishoni, na kusababisha amtoe kwenye wimbo huo, ambao wengi walikuwa hawajui kuwa alishirikishwa Linex.

Bahati aliendelea kusema kuwa alitaka wimbo huo uwe njia ya kutokea kwa Linex nchini kenya, kwa madai kuwa yeye ni msanii ambaye anakubalika sana nchini humo.

“Linex sijui ni msanii wa aina gani, tumepanga video kila kitu nimeboook hadi hoteli, akazingua last minute, unajua muziki at the same time tunafunguliana milango, na mimi nilikuwa nataka hii nyimbo iwe ya Linex kuingia Kenya, kwa hiyo alikuja Kenya nikampa verse akaenda poa, tukapanga video, alianza kunipa excuse kwamba meneja hajabook, na yeye ndiye aliyekuwa akiniambia tupange shoot, unajua mi sasa hivi nimewin three times top male artist, sa hii ingekuwa kwa ajili ya yeye kuingia Kenya”,alisema Bahati.

Planet Bongo iliamua kutoliachia hapo suala hilo, na kuamua kumuendea hewani Linex kumuuliza ilikuwaje mpaka afikie hatua ya kumtosa msanii huyo, ambaye anafanya poa na ngoma yake hiyo ya ‘mapenzi’, na kuwa na haya ya kuileza jamii.

“Kilichotokea ni kwamba nilishindwa kufika kwa sababu mi nakumbuka tumepanga tufanye kazi Jumamosi, mi nikapata kazi ilikuwa inafanyika siku ya Ijumaa, kwa hiyo nikawa na hakika kwamba kwa kuwa imekuwa hivyo, itabidi nipige tu flight asubuhi kabisa, management yangu haikunifanyia booking ya tiketi kwa hiyo nikashindwa kusafiri hiyo Jumamosi kwenda kufanya hiyo video”, alsema Linex

Linex aliendelea kusema kuwa hakufanya kwa makusudi kutoenda Kenya na kufanya hiyo video, kwani hata na yeye anaelewa ni jinsi gani inavyogharimu……..

“Bahati nakumbuka akalalamika sana kwamba mi nishaingia gharama, na mi najua kwa sababu nishafanyaga video zangu, najua ukichelewesha video inakuwa hasara kiasi gani”, alisema Linex

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364