Msanii wa Nigeria awatamani Ali Kiba, Diamond
MSANII wa muziki wa pop kutoka nchini Nigeria, Omo Alhaji Ycee, ametoa msaada wa Sh milioni moja katika kituo cha wanajamii cha Kigamboni Community Center (KCC) ili zisaidie kutokomeza umasikini.
Msanii huyo ambaye yupo katika ziara ya kutangaza muziki wake, aliliambia MTANZANIA kwamba ameamua kuunga mkono kituo hicho kwa sababu ya kujitolea kwao kukuza vipaji na kuendeleza elimu kwa jamii.
Katika hatua nyingine, msanii huyo amedai atafanya mazungumzo na wasanii wanaofanya vizuri nchini katika muziki ili afanye wimbo wa kushirikiana.
“Wasanii ninaotamani kufanya nao wimbo ni Ali kiba na Diamond kwa kuwa wapo katika kiwango cha kimataifa,” alisema Ycee ambaye baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini ataelekea nchini Afrika Kusini.
Mtanzania